Icc yatengua hukumu ya BEMBA
Makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, DRC, Jean Pierre Bemba, amefutiwa hukumu ya Uhalifu wa Kivita na Uhalifu dhidi ya Binadamu,
Mahakama ya ICC imemuondolea hukumu hiyo ambayo awali alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na makosa hayo,
Bemba alikutwa na hatia Machi, 2016 kwa makosa ya uhalifu uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003,
Bemba aliingia matatani akituhumiwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka raia wa Afrika ya Kati,
Wakati anatengua hukumu hiyo, Jaji Christen Van den amesema mwanasiasa huyo hawezi kulaumiwa kwa vitendo vya waasi hao.
No comments