NEW POSTS

MZEE YUSUFU ATEMA YA MOYONI KATIKA MSIKITI WA MTAMBAN

Aliyekuwa msanii nguri katika Tasnia ya uimbaji wa Taarabu maarufu kama Mzee Yusuf

Leo amepata kuzungumza na waumini wa masjidi MTAMBANI baada ya swala ijumaa ambapo Imamu wa msikiti huo sheikh Suleiman

Alimpatia nafasi Mzee Yusuf dakika chache kuzungumza na waislamu walioshwali katika msikiti huo

Katika Yale ambayo amepata kuyazungumza Mzee Yusuf, kuhusiana na hali yake kwa sasa ya kimaisha kulinganisha na hapo awali alipokuwa katika uimbaji wa Taarabu

Lakini pia amesihi wasanii wengine ambao bado nawo hawajaweza kurejea kwa kumuumba wao ili hali wakijua wanayoyafanya sio mazuri, alisema Mzee Yusuf.

Pia aliendelea kuwasihi waumini kuzidisha sana kuwa karibu na mungu wafanye sana istighfar( waombe msamaha) kwa mwenyezi mungu, na wadumishe swala tano

Aliendelea kusema yeye maamuzi yake hayakuwa ni ya nguvu yake Bali ni mwenyezi mungu ndio aliyemsukuma kurudi kwake, lakini

Aliwahidi waumini kuwaletea NASHDI  mpya itakayoenda kwa jina LA happy birthday QUR'AN, hiyo nikutokana na khutba ambayo imezungumzwa katika msikiti huo na imememvutia sana

Lakini mwishoe Mzee Yusuf aliwapatika waumini kwa kuwaimbia nashdi yake mpya ambayo inafanya vizur katika nashdi, ambayo aliimba pamoja na waislamu wote msikitini

Kwa habari za umakini na ufanisi usikose kupitia kwenye blog yako ya Saady Blog.

2 comments:

  1. Replies
    1. Sawa kaka asante kwa mchango wako nazidi kupitia blog yetu uzidi kuhabarika

      Delete