Ufaransa mabingwa wapya wa Kombe la Dunia
NI UFARANSA! Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutwaa kombe la Dunia baada ya kuichapa Croatia magoli 4-2 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jioni ya leo.
Croatia wameshindwa kulipa kisasi kwa Ufaransa ambao waliwatoa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hii mwaka 1998.
Magoli ya Ufaransa yamefungwa na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezman, Kylian Mbappe na kiungo Paulo Pogba huku yale ya Croatia yakiwekwa kimiani na Ivan Perisic pamoja nae Mario Mandzukic.
Hii inakua mara ya pili kwa Ufaransa kutwaa ubingwa huo ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1998 walipoichapa Brazil 3-0 kwenye fainali ambazo waliziandaa wenyewe.
Kocha Didier Deschamps ameweka rekodi yake ya kuwa miongoni mwa walioshinda taji hilo wakiwa wachezaji na baadae makocha. Deschamps alikua nahodha katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa mwaka 1998 na leo hii ameiongoza timu hiyo kutwaa tena ubingwa huo akiwa kocha.
Mchezo huo umehudhuriwa na marais wa mataifa yote mawili sambamba na mwenyeji wao Vladimir Putin.

No comments